STANDARD 7 TERMINAL EXAMS SERIES


EXAM SERIES EXAM

OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
SAYANSI - MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
DARASA LA SABA
MUDA: 1.30
MAELEKEZO
 1. MTIHANI  HUU UNA MASWALI 50
 2. JIBU MASWALI YOTE KWENYE NAFASI YA KARATASI ULIOPEWA
 3. HAKIKISHA KAZI YAKO NI SAFI
 4. DUMISHA UAMINIFU KATIKA KAZI YAKO.
SEHEMU A. CHAGUA JIBU SAHIHI KUTOKA YALE ULIOPEWA.
1. Usafirishaji wa chakula mwilini hufanywa na: 
 1. moyo     
 2. damu
 3. misuli                                     
 4. mapafu
 5. maji
2. Tazama kwa makini kielelezo namba 2 kisha jibu maswali yanayofuata:

Alama Y inawakilisha sehemu iitwayo:
 1.  petali
 2.  filamenti
 3.  chavulio
 4.  pistili
 5.  ovari
3. Lipi kati ya magonjwa yafuatayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana?
 1.  Polio  
 2.  Kipindupindu         
 3.  Pepopunda
 4.  Kaswende                            
 5.  Tetekuwanga
4. Lipi kati ya mafungu yafuatayo ya vyakula hulinda mwili?
 1.  Samaki na maziwa          
 2.  Ugali na ndizi
 3.  Maharagwe na karanga 
 4.  Mayai na kabichi 
 5.  Matunda na mboga za majani
5. Umuhimu wa asidi ya haidrokloric katika tumbo ni:
 1.  kubadili hali ya besi katika tumbo
 2.  kulainisha mafuta tumboni
 3.  kuongeza uchachu tumboni
 4.  kumengenya vyakula vya sukari tumboni 
 5.  kuua wadudu wanaoingia tumboni na chakula.
6. Kipi kati ya vifuatavyo vinapaswa kudumishwa? 
 1. Kutumia kikombe kimoja wakati wa kunywa maji. 
 2. Kunawa mikono kabla ya mlo katika karai moja. 
 3. Kupika mboga za majani na nyama kwa muda mrefu.
 4. Kuchemsha na kuchuja maji ya kunywa. 
 5. Kuogelea katika mito na mabwawa.
7. Mbungo husababisha ugonjwa uitwao ....
 1.  homa ya matumbo     
 2.  nagana
 3. malale                                           
 4. matende                
 5. homa ya ini
8. Tunaweza kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya yafuatayo: .......
 1. Kula chakula na kufanya mazoezi mara kwa mara
 2.  Kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka kuvuta sigara na kuepuka kunywa pombe
 3.  Kula chakula chenye chumvi na kunywa pombe 
 4. Kufanya mazoezi ya mwili na kuvuta sigara 
 5. Kula vyakula vyenye mafuta na kunywa pombe
9. Ili kujikinga dhidi ya malaria ni muhimu .........
 1.  kumeza mchanganyiko wa madawa
 2.  kutumia dawa za mitishamba
 3.  kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa
 4.  kujifunika na blanketi Zito lililowekwa dawa 
 5.  kufanya mazoezi kila mara
10.  Mojawapo ya kazi za misuli katika mwili ni:
 1.  kuwezesha kujongea
 2.  kuruhusu damu kupita 
 3.  kuruhusu maji kupita
 4. kuruhusu hewa kupita 
 5.  kuimarisha mwili
11.  Lipi kati ya mambo yafuatayo si sahihi kumfanyia mtu aliyebanwa misuli?
 1.  Kuchua eneo lililoathirika kwa kiganja
 2.  Kuchua kwa kukandamiza eneo lililoathirika hadi misuli ilegee
 3.  Kuuchua msuli kwa kitambaa na maji baridi 
 4.  Kuweka kemikali zitakazowezesha misuli kulegea
 5.  Kulala juu chini na kuchua msuli ulioathirika kvva maji moto.
12. Huduma ya kwanza anayopewa mtu aliyezimia ni:
 1.  kumpa hewa ya oksijeni
 2.  kumpa juisi ya nazi mbichi
 3.  kumlaza juu chini na kumbonyeza tumbo
 4.  kumpa maji yaliyochanganywa na glukosi
 5.  kumpa juisi ya malimao, sukari na chumvi
13. Mtandao wa watu wenye virusi vya UKIMWI unatanuka kwa kuwa
 1.  matumizi ya kondom na simu za mkononi yameongezeka
 2.  matangazo kuhusu UKIMWI yameboreshwa
 3.  kuna ongezeko la mahusiano ya kingono yasiyo salama
 4.  elimu ya UKIMWI inatolewa kwa watu wachache
 5.  watu wenye UKIMWI wanazingatia kanuni za kujikinga na UKIMWI
14.     Mwanga hupinda unapopita kutoka
 1.  Ncha ya Kaskazini kwenda Kusini      
 2.  media moja kwenda nyingine
 3.  Ncha ya Kaskazini kwenda Mashariki 
 4.  Magharibi kwenda Mashariki 
 5.  Kaskazini kwenda Magharibi

15.     Hewa ya kabonidaiyoksidi hutumika kuzima moto kwasababu:

 1.  haichochei uwakaji
 2.  ni nzito kuliko hewa
 3.  haiwaki
 4.  hunyonya joto
 5.  huungana na oksijeni
16. Mifupa imeundwa kwa madini ya:
 1.  Sodiamu na kalsiamu
 2. Kalsiamu na oksijeni
 3. Fosforasi na kalsiamu 
 4.  Salfa na fosforasi
 5.  Kalsiamu na chuma 
17.    Sumaku inaweza kuvuta vitu vyenye asili ya:
 1.  mpira     
 2.  udongo  
 3.  madini  
 4. karatasi 
 5. chuma
18.Katika kurunzi, nishati ya umeme inayotoka kwenye betri hubadilishwa na kuwa:
 1.  nishati ya kikemikali  
 2.  nishati ya joto
 3.  nishati ya kimakaniki     
 4.  nishati ya mwanga 
 5.  Nishati ya moto
19.Mojawapo ya hatua za kufuata unapoandaa jaribio la kisayansi ni: 
 1.  uchunguzi    
 2.  udadisi
 3.  utambuzi wa tatizo    
 4.  utatuzi wa tatizo
 5.  kuandaa ripoti
20.  Lipi kati ya magonjwa yafuatayo husambazwa na inzi na mende? 
 1. Tetekuwanga   
 2. Kuhara        
 3. Kifaduro
 4. Utapia mlo 
 5. Homa ya matumbo
21. Lipi kati ya yafuatayo linapaswa kuzingatiwa kabla ya kumhudumia mgonjwa wa UKIMWI?
 1.  Vaa nguo safi 
 2.  Nawa kwa sabuni 
 3.  Vaa glovu 
 4.  Sali 
 5.  Mruhusu apumzike

22. Kiwango cha maji kinachopotezwa na mmea huathiriwa na hali za hewa zifuatazo...

 1.  joto na unyevu     
 2.  unyevu na mwanga
 3. upepo na mwanga wa jua               
 4.  mawingu na upepo
 5. unyevu na upepo
23. Tunaweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi kwa kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo:
 1. Kukata miti
 2. Kuongeza mbolea kwenye udongo
 3. Kuotesha nyasi 
 4.  Kuweka matuta lavenye maeneo ya mteremko
 5.  Kupanda miti 
24.   Tazama mchoro ufuatao unaoonesha sehemu za ndani za mbegu ya haragwe....

Ni sehemu ipi inayohusika na kuilinda mbegu isiharibiwe na wadudu waharibifu mabadiliko ya jotoridi? 
 1. 2
 2. 3
 3. 5
 4. 4
 5. 1
25. Hatua ya kwanza ya utafiti wa kisayansi ni 
 1.  kuanza jaribio 
 2. kukusanya data
 3.  kutambua tatizo   
 4.  kuchanganua data
 5.  kutafsiri matokeo
26. Bahati aliweka karatasi nyekundu ya litmus kwenye myeyuko asioutambua. Rangi ya karatasi ya litmas ilibadilika na kuwa bluu.Hii inaonesha kuwa myeyuko ule ulikuwa .........
 1.  asidi 
 2.  besi 
 3.  maji 
 4.  mafuta  
 5.  spiriti
27.Nini kitatokea iwapo ncha mbili za KASKAZINI za sumaku zitaletwa pamoja?
 1.  Zitavutana kwa nguvu
 2.  Zitavutana kuelekea upande mmoja
 3.  Zitasukumana
 4.  Hakuna kitakachotokea
 5.   Zitavunjika
28. Dhana ya kuakisiwa kwa mwanga inadhihirika katika moja ya vifaa vifuatavyo: 
 1.  Hadubini 
 2.  Televisheni 
 3.  Saa
 4.  Balbu 
 5.  Miwani
29.  Ipi kati ya vifuatavyo huzunguka dunia toka magharibi kwenda mashariki?
 1. Jua    
 2. Nyota 
 3. Mwezi
 4.  Kimondo  
 5. Sayari
30. Mojawapo ya kazi za mifupa ni kutengeneza:
 1.  seli visahani 
 2.  plasma
 3.  selihai nyeupe  
 4. selihai nyekundu
 5.  selihai za kugandisha damu
31. Uhuru ana tatizo la meno yanayovunjika na miguu dhaifu. Ni virutubisho gani utamshaufi atumie ili kutatua tatizo lake hili?
 1.  Madini ya chuma           
 2.  Madini ya fosforasi
 3.  Madini ya kasiamu   
 4. Madini joto
 5. Vitamini K
32. Kazi ya uta mgongo katika mfumo wa fahamu wa mwanadamu ni
 1.  Kuongoza matendo ya hiari   
 2.  kuongoza matendo yasiyo ya hiari 
 3.  Kuongoza miondoko ya mwili  
 4.  kudumisha umbo la mwili 
 5.  kupeleka taarifa katika mfumo mkuu wa fahamu.
33. Katika hali ya kawaida, kutu ni matokeo ya mjibizo wa athari za kikemikali kati ya:
 1.  shaba, maji na oksijeni  
 2.  sodiamu, maji na oksijeni
 3.  kalsiamu, maji na oksijeni    
 4.  chuma, oksijeni na maji 
 5.  maji, oksijeni na potasiamu
34. Njia zifuatazo huweza kutumiwa kuhifadhi vyakula na mazao ili visiharibike ISIPOKUWA:
 1.  kuoka  
 2.  kutumia asali
 3.  kukausha    
 4.  kutumia chumvi 
 5. kutumia maji
35.  Yafuatayo ni makundi ya vyakula isipokuwa:
 1.  madini ya chumvi chumvi  
 2.  vitamini
 3. Maji   
 4. protini 
 5. hamirojo
36. Mlishano sahihi ni:
 1. Mwewe  Nyasi  Chui  mbuzi 
 2.  Nyasi  Mwewe  chui  mbuzi
 3.  Chui    Mwewe  Nyasi  mbuzi
 4. Nyasi  mbuzi  chui    mwewe
 5. Mwewe  chui  mbuzi  nyasi 
37. Sehemu tatu kuu zinazounda mfumo wa damu ni:
 1.  ateri, vena na kapilari
 2.  damu, moyo na mapafu
 3.  damu, mishipa ya damu na moyo
 4.  mishipa ya damu, moyo na valvu 
 5.  moyo, aota na ateri
38.  Matatizo katika mfumo wa uzazi wa wanawake hutokana na upungufu wa hol zifuatazo 
 1. Pituitari na insulin
 2. Estrojen na projesteron
 3. Thyroksin na pituitari
 4. Estrojen na insulin
 5.  Thairoksin na estrojen
39. Lipi kati ya makundi yafuatayo ni sifa zinazotumika kutambua wanyama wa kundi la reptilia?
 1. Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kuishi majini. 
 2. Kutaga mayai, kuishi majini na kuishi nchi kavu.
 3. Kutaga mayai, kuwa na damu ya joto na kuishi nchi kavu.
 4.  Kutaga mayai, kuwa na damu baridi na kupumua kwa kutumia mapezi.
 5. Kutaga mayai, kupumua kwa kutumia ngozi na kuishi majini.
40. Kukosekana kwa chanikiwiti katika mmea huweza kusababisha:
 1. mmea kukosa madini joto
 2. mmea kushindwa kusanisi chakula
 3. majani ya mmea kukauka 
 4. majani ya mmea kuwa njano
 5. maj ani ya mmea kupukutika.
41. Sehemu ya chembe hai inayohusika na kutawala shughuli zote za chembe hai huitwa:
 1. saitoplazimu 
 2. vakuoli
 3. kloroplasti 
 4. kiwambo cha seli
 5. nyukliasi
42. Sehemu ya kike ya ua inayohusika na uzazi ni:
 1. stameni 
 2. staili 
 3. ovari
 4. Petali
 5. Sepali
43. Tofauti kati ya tunda na mbegu ni: 
 1. Mbegu ina tunda.
 2. Tunda huota.
 3. Tunda lina kotiledoni mbili. 
 4. Mbegu huota. 
 5. Mbegu haziliwi.
44. Vyakula vyenye kabohaidreti huwezesha mwili:
 1. kuhimili magonjwa
 2. kuwa na joto
 3. kukua kwa haraka 
 4. kuwa na nguvu 
 5. kuwa mwororo
45. Mapumziko baada ya kazi ni muhimu kwa sababu gani?
 1. Mwili hupoa. 
 2. Mwili hutulia.
 3. Mwili hurejesha nishati. 
 4. Mwili hufanya shughuli nyingine.
 5. Mtu hupata fursa ya kulala.
SEHEMU B. Jaza nafasi zilizowazi kwa kutoa majibu mafupi.
46. (a) Taja mahitaji mawili muhimu kwa ukuaji wa mimea
      (b) Mapacha wanaofanana wanatokana na nini…………………
47.  Sumaku ni nini?
48. Eleza matumizi ya sumaku
49. Mkondo waumeme unapimwa na kifaa kinaitwa………………………..
50. Kizio cha mkondo wa umeme ni? ..............................................


STANDARD SEVEN SAYANSI EXAM SERIES 9
OFISI YA RAIS WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI- MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
DARASA LA SABA
MUDA: 1.30                                                        DARASA LA VII
MAELEKEZO
 1. Karatasi hii ina kurasa nne zenye maandishi yenye sehemu A,B, C,D na E zenye maswali arobaini na tano (45).
 2. Jibu maswali yote katika kila sehemu ya mtihani huu.
 3. Kumbuka kuandika majina yako, na shule yako kwenye karatasi ya kujibia.
 4. Hakikisha kazi yako ni nadhifu sana.
 5. Tumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi kwa maswali yote uliyopewa.
SEHEMU : A SARUFI
Chagua herufi ya jibu sahihi kisha uiandike kwenye karatasi ya kujibia uliyopewa
1. Wingi wa neon uteo ni nini?
 1. Mateo
 2. Teo
 3. Uteo
 4. Mauteo
 5. Lungo.
2. Kitenzi “anapigwa” kipo katika kauli gani?
 1. Kutenda
 2. Kutendwa
 3. Kutendewa
 4. Kutendeka
 5. Kutendesha
3. Wingi wa neon “paka” ni ipi?
 1. Mipaka
 2. Paka
 3. Mapaka
 4. Vipaka
 5. Wapaka.
4. Kisawe cha neon bahati ni kipi kati ya maneno yafuatayo?
 1. Tunu
 2. Sudi
 3. Shani
 4. Hiba
 5. Hidaya
5. Ni neon lipi kati ya haya yafuatayo halilandani na mengine?
 1. Fikiri
 2. Dodosa
 3. Uliza
 4. Hoji
 5. Saili
6. Juma aliondoka hivi punde; maneno “hivi punde” yanamaana gani?
 1. Haraka
 2. Muda mrefu
 3. Karibuni
 4. Kwa pupa
 5. Kwa haraka
7. Sweta langu limeshonwa na fundi mzoefu, “mzoefu” ni aina gani ya neon?
 1. Kielezi
 2. Kivumishi
 3. Kiunganishi
 4. Nomino
 5. Kitenzi
8. Mlinzi wa mlango huitwaje?
 1. Boharia
 2. Baharia
 3. Bawaba
 4. Banati
 5. Bawabu
9. Neno lipi tofauti na mengine katika maneno yafuatayo?
 1. Maji
 2. Maziwa
 3. Soda
 4. Juisi
 5. Samli
10. Nywele zinazoota kuanzia kwenye maskio mpaka kwenye mashavu huitwa?
 1. Mvi
 2. Sharafa
 3. Ndevu
 4. Sharubu
 5. Kope
11. Sehemu ngo’mbe huogeshwa hili kuwaepusha na magonjwa hutwa?
 1. Mto
 2. Ziwa
 3. Bwawa
 4. Josho
 5. Joshi
12. Joshua yupo jikoni anapaa samaki. Neno anapaa kama lilivyo tumika katika sentensi lina maana gani?
 1. Kuwapaka samaki chumvi
 2. Kuondoa magamba ya samaki
 3. Kuondoa mifupa katika samaki
 4. Kukausha samaki kwa moto
 5. Kuwakata samaki vipande vipande.
13. Siku ya nne baada ya leo huitwa?
 1. Mtondo
 2. Mtondo kutwa
 3. Mtondogoo
 4. Kesho kutwa
 5. Mtondogoo kutwa
14. Msemo usemao “kushikwa sikio” una maana ipi?
 1. Kusemwa
 2. Kunong’onezwa
 3. Kuelezwa
 4. Kusengenywa
 5. Kuonywa
15. “Bwana mkubwa amelala ndani lakini ndevu zipo nje zapepea” Jibu sahii la kitendawili hiki ni
 1. Ulezi
 2. Mpunga
 3. Ngano
 4. Mahindi
 5. Mtama
16. Kisawe cha eupe ni kipi?
 1. Chokaa
 2. Angavu
 3. Theluji
 4. Ukunga
 5. Angaza
17. Kimatu ni motto wa nani?
 1. Nzige
 2. Nyuki
 3. Inzi
 4. Kipepeo
 5. Buibui
18. Kitenzi “piga” kikiwa katika hali ya kutendeka kitakua neon lipi?
 1. Pigia
 2. Pigwa
 3. Pigika
 4. Pigiwa
 5. Pigana
19. “Sote tunafanya mtihani darasani” Neno darasani limetumika kama aina gani ya neon?
 1. Kielezi
 2. Kivumishi
 3. Kitenzi
 4. Kiwakilishi
 5. Nomino
20. Ni sentensi ipo sahii kimuundo katika zifuatazo?
 1. Amenunua gari mashaka
 2. Mashaka gari amenunua
 3. Amenunua mashaka gari
 4. Mashaka amenunua gari
 5. Gari amenunua mashaka.
SEHEMU B. LUGHA YA KIFASIHI.
Katika swali la 21-30, andika jibu sahili la kila swali.
21. Watoto wa mfalme ni rahisi kujificha” Jibu la kitendawili hiki ni………..
 1. Macho
 2. Vifaranga
 3. Siafu
 4. Mvi
 5. Sungura
22. Kamili methali. “Heri kufa macho kuliko…………
 1. Kujikwaa ulimi
 2. Kuumia moyo
 3. Kuzama majini
 4. Kufa moyo
 5. Kufa jicho moja
23. Anatengeneza mchuzi mtamu sana lakini hapiki jikoni. Lipi jibu la kitendawili hiki?
 1. Ng’ombe
 2. Nyuki
 3. Mbuzi
 4. Muwa
 5. Kuku
24. Nimeugua kwa muda mrefu sana, lakini sasa ni…………wa afya. Neno lipi linakamilisha sentensi hii?
 1. Hoi
 2. Buheri
 3. Buheli
 4. Mzuri
 5. Mwingi
25. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?
 1. Mbalika
 2. Nzi
 3. Mhindi
 4. Embe
 5. Mtama
26. Kamilisha methali hii.Mwamba ng’oma……………
 1. Hualika watu wengi
 2. Hufanya maandalizi mengi
 3. Huimba nyimbo nyingi
 4. Ngozi huvutia kwake
 5. Hucheza na jamaa zake
27. Tegua kitendawili kifuatacho. “Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji”
 1. Kikombe
 2. Kata
 3. Kinywa
 4. Kibatari
 5. Mtungi
28. Ni methali ipi kati ya hizi inafanana na isemayo, mwenda pole hajikwai?
 1. Haba na haba hujaza kibaba
 2. Fuata nyuki ule asali
 3. Awali ni awali hakuna awali mbovu
 4. Mchumia juani hulia kivulini
 5. Baada ya dhiki faraja
29. Methali isemayo, “mgaagaa na upwa hali wali mkavu inatoa funzo gani?
 1. Bidii huleta maafanikio
 2. Mafanikio ni matokeo ya kazi
 3. Bidii huleta faraja
 4. Bidii ni kazi ya kuhangaika
 5. Mafanikio ni ya lazima.
30. Methali ipi kati ya hizi  haitoi onyo kuhusu tabia ya mtu?
 1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
 2. Kiburi si maungwana
 3. Motto mkaidi mngoje siku ya ngoma
 4. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi
 5. Mt0to mwerevu hafunzi adabu
SEHEMU C. UFAHAMU.
Soma kifungu kifuatacho kwa makini kasha jibu maswali 31-40.
Jua lilikuwa linaunguza mithili ya moto. Hapakuwa na nyasi wala miti iliyokuwa na majani ya rangi ya kijani.Kila uoto ulikuwa wa rangi ya kahawia kavu! Aidha kupata tone la maji ya kunywa ilikuwa ndoto kwani mito na visima vyote vilikauka kau.Baada https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image073.jpgkuhangaika kwa njaa na kiu, ndipo wanyama waliamua waitishe mkutano ili wajadili hatua ya kuchukua. Makundi • ya wanyama wa aina mbalimbali walikutana chini ya mbuyu. Swala, nyani, mbawa na tembo wote walikuwepo.
"Kama mjuavyo mimi ndimi mfalme wa wanyama wote.Niungurumapo hapana achezae kwa hiyo bila shaka mtakubali kuwa mimi ndiye mwenyekiti wa mkutano huu."alitangaza simba.Wanyama wote walitazamana na kutikisa vichwa kwa ishara ya kuafiki. Kisha alisimama na kusema "Mheshimiwa mwenyeki├║, jana nilisikia mlindimo toka upande wa magharibi. Hivyo ninashauri sote tuhame na kuelekea upande huo ili tuokoe maisha yetu kwani huko kuna dalili ya mvua."Wanyama wote waliunga mkono hoja hiyo,isipokuwa kobe ambaye alisema, "mheshimiwa mwenyekiti, endapo kweli tumeazimia kuhama, sisi akina kobe tunaomba mtubebe kwani kasi yetu ya kutembea ni ndogo mno."
Baada ya kila mnyama kutoa rai yake ,Mwenyekiti alisimama na kusema, "Nimesikia yote mliyosema, kabla ya kuanza kuhama nakutuma wewe ngombe upeleke ujumbe wetu kwa binadamu ili waache kuharibu mazingira, kwani hicho ndicho kiini cha matatizo yanayotusibu.Wewe ni kiungo baina yetu na binadamu." ngombe alikubali.
Baada ya kufika ujumbe ule, binadamu alijibu kuwa alikwishaelewa tatizo Ia mazingira na tayari alikuwa na mpango kabambe wa kuchinja mifugo yote ili kutekeleza ushauri wa wataalamu wa mazingira wa kuiokoa dunia na janga Ia jangwa. Kusikia hivyo ngombe alichanja mbuga kuelekea kwa wanyama wengine.
31.  Kwa mujibu wa habari uliyo soma, mkutano wa wanyama ulifanyika wapi?
 1. Kwa mfalme
 2.  Kisimani
 3. Chini ya mbuyu D. 
 4. Kwenye majani
 5. Jangwani.
32.  Mwenyekiti wa mkutano wa wanyama alikuwa nani?
 1. Ng ombe
 2.  Kobe
 3. Nyati
 4. Simba
 5. Nyani
33. Hali ya kukauka kwa mito,visima nyasi na miti kunakutokana na ukosefu wa mvua inaitwaje?
 1. Ukame
 2. Uoto https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image049.jpg
 3.  Kahawia https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image011.jpg
 4.  loto
 5. Janga.
34. Jina lingine Ia mnyama aliye washauri wanyama wote kuhamia upande ambako kulikuwa na dalili ya mvua ni lipi kati ya https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image042.jpgyafuatayo.
 1.  Ndovu B.
 2.  Ngwena
 3. Mbega 
 4.  Kima
 5. Mbogo.
35.Katika habari uliyo soma sababu iliyomfanya kobe kutoafiki moja kwa moja hoja ya kuhama ni ipi?
 1. alikuwa mpinzani wa mwenyekiti ,
 2. aliogopa kuachwa nyuma, https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image022.jpg
 3. kulikuwa na jua kali
 4. wanyama wengine wangeweza kumla,
 5. kobe ni mvivu kutembea.
36. kwa mujibu wa habari hii ,uharibifu mkubwa wa mazingira hufanywa na nani?
 1. tembo
 2.  mbawala
 3.  swala https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image083.jpg
 4. binadamu
 5.  nyani.
37. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno janga?
 1. Maafa 
 2.  Kiu https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image062.jpg
 3. Ukame 
 4. angwa 
 5. Joto.
38.  Kifungu cha maneno "alichanjambuga"kinamaana gani?
 1. Alijirudi
 2. Alitembea
 3. Alikimbia
 4. Alirudi https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image056.jpg
 5. Aliruka
39.  Binadamu alikusudia kuchinja wanyama wa aina gani
 1. Wanyama pori wote
 2. Ngombe na simba  https://myfiles.space/user_files/30996_4958b541bbe404eb/1569855423_kiswahili-2017_files/image056.jpg
 3. Wanyama wadogo wote
 4. Wanyama wakubwa wote
 5. Wanyama wote wanaofugwa
40.  Kichwa cha somo uliyosoma kingefaa kiwe kipi?
 1. Kiangazi na jangwa
 2. Matatizo ya binadamu
 3. Jua kali
 4.  Uhamisho wa wanyama
 5. Uharibifu wa mazingira 
SEHEMU D. USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuweka kivuli katika herufiya jibu.
Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali,
Mule wanamotangaza, matangazo lugha mbili, Juu kuwa Kingereza, Chini kuwa Kiswahili, Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.
Kitangazwe Kingereza, baada ya Kiswahili
Hivi tutapotimiza, lugha itakuwa ghali,
Hivi mnavyofanyiza, sana mnaidhalili,
Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza
Serikali bembeleza, tafakari tafadhali,
Jambo hili kueleza, kwa zingine serikali Kiswahili kutangaza, kuwa Chini twakidhili Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.
Tuache kukipumbaza, kwa andiko au kauli, Kwa nyuma kukisogeza, kukipa kisulisuli,
Lazima kuyafukuza, yawezayo kikatili,
Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza
Na wenyewe kujikaza, kwa bidii za kimwili kiswahili kutukuza, tukivalie bangili,
Ngomani kutumbuiza, waume na wanawali Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.
41. Katika shairi hilo mstari wa pili katika ubeti wa pili una mizani mingapi?
 1. Tano
 2. mbili
 3. kumi na sita
 4. nane
 5. thelathini na tatu
42. Katika ubeti wa nne, vina ni vipi?
 1. Za na li 
 2. La na li
 3. La na ya
 4. Ju na za
 5. Tu na li
43.      Kituo ni kipi katika shairi hili?
 1. Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali
 2.  Kitangazwe Kingereza, badala ya Kiswahili 
 3. Serikali bembeleza, tafakari tafadhali
 4. Tuache kukipumbaza, kwa andiko na kauli
 5. Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza
44.      Shairi hili linahimiza kuhusu nini?
 1. Kudumisha na kuendeleza mila
 2. Kudumisha na kuendeleza jadi zetu
 3. Kudumisha lugha ya Kingereza
 4.  Kudumisha na kuendeleza Kiswahili 
 5.  Kudumisha na kuendeleza lugha
45.      Ujumbe unaopatokana katika shairi hili unafanana na methali ipi?
 1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
 2.  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
 3. Mkono usioweza kuukata ubusu. 
 4.  Ukitaka cha uvunguni sharti uiname.
 5. Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.
46.      Kutokana na shairi ulilosoma neno "kutukuza” lina maana ipi?
 1. Shutumu 
 2.  Laumu
 3. Heshimu 
 4. Fadhaisha
 5. Kasirisha
 SEHEMU D. UTUNGAJI
Panga sentensi nne (4) zifuatazo hili ziwe kwa mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B,C na D.
47. Zizi hilo limegawanywa katika sehemu mbili
48. Baba yangu anafuga mbuzi Ng’ombe na kondoo
49. Nje ya nyumba yetu kuna zizi kubwa
50. Sehemu moja ni ya ngo’ombe na nyingine ni ya mbuzi na kondoo.


STANDARD SEVEN KISWAHILI EXAM SERIES 8
THE PRESIDENT’S OFFICE MINISTRY OF EDUCATION, LOCAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
ENGLISH- TERMINAL EXAMINATION-MAY
STD SEVEN
TIME: 1.30 HRS                                                   2020
NAME:_________________________________CLASS:___________
          INSTRUCTIONS
 1. This paper consists of three sections A, B,C and D
 2. Answer all questions in all sections
 3. All answers should be written in spaces provided
 4. Ensure clarity in your work
SECTION   A.  GRAMMAR.
Choose the words that complete the sentences by shading the letters of the correct answer.
1. He always ………………………………..when he was young
 1. Cry
 2. Cries
 3. Cried
 4. Crying
 5. Does cry
2. The snake………………….by Mrs. Mwenda
 1. Was killed
 2. Had killed
 3. Were killed
 4. Was kill
 5. Have killed.
3. If you…………….hard you will pass your examinations
 1. Work
 2. Worked
 3. Had worked
 4. Was working
 5. Works
4. My brother’s daughter is my………………………..
 1. Nephew
 2. Child
 3. Niece
 4. Uncle
 5. Daughter
5. The girl…………….came here yesterday is my daughter
 1. Which
 2. Whose
 3. What
 4. Whom
 5. Who
6. Most children go to school…………………….foot
 1. By
 2. With
 3. Using
 4. In
 5. On
7. Girls like to go out alone at night……………………….
 1. Are they?
 2. Do they?
 3. They do?
 4. Aren’t they?
 5. Don’t they?
8. Arusha and Dar es salaam are ………………………..business centers
 1. All of
 2. More of
 3. Either 
 4. Both
 5. Each.
9. The headmaster has been waiting for the watchman ………………one hour
 1. Since
 2. For
 3. Against
 4. Fore
 5. Until
10. My father ………..the car he bought
 1. Was shown
 2. Show
 3. Has shown
 4. Are showing
 5. Is shown.
11. Many people………………….cassava next season
 1. Is planting
 2. Are planting
 3. Are planted
 4. Will plant
 5. Was planting.
12. Our sister………………….her left leg last year.
 1. Is breaking
 2. Broke
 3. Will broke
 4. Was breaking
 5. Has broken
13. My car looks dirty but yours looks …………
 1. More dirty
 2. Dirtiest
 3. Dirtier
 4. Most dirty
 5. Dirty.
14. Usually the sun …………in the west..
 1. Sank
 2. Is sinking
 3. Sinks
 4. Was sinking
 5. Sunk.
15. Dan is a slow driver. He …………to drive more carefully.
 1. Should
 2. Could
 3. Would
 4. Ought
 5. Shall.
16. The books…………………….on the shelf
 1. Were arranged
 2. Was arranged
 3. Were arranging
 4. Arrange
 5. Arranges.
17. The national football team…………….won the match.
 1. Is
 2. Are
 3. Were
 4. Has
 5.  Shall
18. Many living things are ...............animals or insects
 1. Both
 2. Too
 3. Either
 4. Neither
 5. As
19. The pen on the desk belongs to me, so it is
 1. imagehers
 2. his
 3. imagetheirs
 4. mine
 5. my
20. The fire that ..................       the whole village started from here.
 1. destroys
 2.  destroyed
 3. destroying
 4. will destroy
 5. have destroyed
21.The fire that ..................       the whole village started from here.
 1. destroys
 2.  destroyed
 3. destroying
 4. will destroy
 5. have destroyed
22.The fire that ..................       the whole village started from here.
 1. destroys
 2.  destroyed
 3. destroying
 4. will destroy
 5. have destroyed
23.imageThe girl who picked flowers started with the...................   beautiful to the least beautiful ones.
 1. ore 
 2. most
 3. less 
 4. not very
 5. a little
24. Chausiku does all the home work   ... she wants to be first in class.
 1. Inspite of
 2. despite
 3. even
 4. but
 5. because
25. The lazy pupils _____________ their homework.
 1. have not did
 2. has not done
 3. have not do
 4. have not done
 5. have did
 26. Every year, Tanzania ___________ a lot of visitors from different countries all over the world.
 1. has taken
 2. will take
 3. shall take
 4. take
 5. have taken
27. He will not pass his examination _____________ he works hard
 1. but
 2. because
 3. even
 4. unless
 5. and.
28. David and Willy were preparing _____________ to go to school.
 1. themself
 2. themselves
 3. theirselves
 4. yourselves
 5. ourselves
29.My sister has bought _____________new dress.
 1. it
 2. you
 3. she
 4. he
 5. her
30. The patient had died ……………….lack of water
 1. with
 2. by
 3. from
 4. of
 5. for.
SECTION B. VOCABULARY.
31. A person who meants shows is called
 1. Shoe maker
 2. Tailor
 3. Sewer
 4. Cobbler
 5. Pedestrian
32. A gun is a ……………………..
 1. Weapon
 2. Fire work
 3. Fire wood
 4. Hot pot
 5. Knife.
33. A person who tests and treats people eyes is called
 1. An eye doctor
 2. A chemist
 3. An optician
 4. A surgeon
 5. A dentist
34. A doctor works in a………………..
 1. Shop
 2. Court
 3. Church
 4. Hospital
 5. Farm
35. Gold, diamond and tanzanite are……….
 1. Chemical
 2. Medicines
 3. Liquids
 4. Minerals
 5. Ores
36. A group of birds flying together is called;
 1. Troop
 2. Flock
 3. Herd
 4. fleet
 5. bunch
37. He cuts and sells meat……………..
 1. Doctor
 2. Butchery
 3. Butcher
 4. Shopkeeper
 5. Seller
SECTION C. COMPOSITION WRITING,
Arrange the following sentences to give a meaningful sentences by giving them letters A-D.
38. While in Dar es salaam, they wrote about what they have seen
39. When they returned home, they told their friends about their enjoyable journey
40. Ali and his friends were excited by their trip to Dar es salaam Trade Fair
41. At the fair, they saw a lot of displays
              SECTION D. COMPREHENSION
Read the following passage carefully and then answer the questions that Follow.
Lilato had a dream. He dreamt that someone gave him an egg. He was very happy and started wondering what to do with it. He thought of either eating it or keeping it in his pocket so that it would be warm and finally hatch and become a chick.
He thought of how this chick would grow into a hen and lay more eggs which will also hatch into more chickens. He would then sell some of those chickens and become a rich man. After getting a lot of money, Lilato thought of building an iron roofed house with glass windows. It would be a beautiful and big house.
While dreaming, Lilato walked excitedly. He jumped and the egg fell from his pocket and broke. He cried, saying that he will never be a rich man. Suddenly, he woke up and thanked God that it was only a dream.
42. Lilato decided to……………………the eggs
 1. Keep
 2. Sell
 3. Hide
 4. Eat
 5. throw
43. The people usually dream when they are………………….
 1. Sleeping
 2. Walking
 3. Sitting
 4. Resting
 5. Wondering
44. Lilato was happy because he was given;
 1. A big house
 2. Iron sheets
 3. A chicken
 4. An egg
 5. A chick.
45. Lilato thought he could get a lot of money by;
 1. Selling eggs and chicken
 2. Building a big house
 3. Selling a big house
 4. Keeping a big house
 5. Keeping eggs.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

buttons=(Accept !) days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !